Rais Samia awaonya wanaofanya urasimu kwenye utoaji wa Visa

HomeKimataifa

Rais Samia awaonya wanaofanya urasimu kwenye utoaji wa Visa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza maafisa wanaoshugulikia hati za kumruhusu mtu kuingia nchini (VISA) kuacha urasimu na kuhakikisha utoaji wa Visa hizo unazingatia maadili.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Uhamiaji Kozi na. 1/2022, katika Chuo cha Uhamiaji Boma Kichakamiba, Rais amesema kutokana na ongezeko la wageni nchini, maafisa hao wanapaswa kuhakikisha hati hizo zinatolewa kwa ufanisi na sio urasimu.

“Mbali ya filamu ya Royal Tour kupitia demokrasia ya kiuchumi nchi yetu tumeifungua sana. Wageni watakuja kwa wingi sana, wawekezaji watakuja kwa wingi sana na kwahiyo ningependa kupendekeza…punguzeni urasimu kwa aina zote za visa,”amesema Rais Samia Suluhu.

Pia amesema wale wote watakaojihusisha na ucheleweshaji wa hati hizo washughulikiwe pamoja na wanaokwepa visa hatua ichukuliwe dhidi yao.

Mbali na hayo, Rais Samia ameshauri kwamba vijana wanaomaliza katika chuo hiko wanaotoka Zanzibar wapangiwe vituo bara ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa kile alichoeleza kwamba, mtu anapokua nyumbani anashindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wabara wapelekwe Zanzibar na vivyohivyo wa Zanzibar.

“Jeshi hili ni jeshi la muungano, lakini kuna kawaida wakisha kuhitimu Wazanzibar wanapashindwa boti haya nendeni kwenu Zanzibar na wengine wanarudi huku. Nataka kusema hawa ni maafisa uhamiaji wa Muungano wanatakiwa kufanya kazi sehemu yeyote ya Tanzania, naingependeza zaidi wale wa Zanzibara wakapangwa Bara na wabara wakapangwa Zanzibar ili kuondosha yale mazoea.” amesema Rais Samia Suluhu.

 

error: Content is protected !!