Rais Samia ateua na kutengua

HomeKitaifa

Rais Samia ateua na kutengua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Oktoba amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi kadhaa kama ifuatavyo.

Rais Samia amemteua Mh. Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Kabla ya uteuzi huo Mh. Mjema alikuwa Mkuu wa wilaya wa Arusha.

  > Serikali kuongeza ndege nyingine 5

Pia amemteua Mh. Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Makungu alikuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Rais Samia pia amefanya uteuzi wa Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huo Jaji Siyani alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Eliner Feleshi aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huo umeanza tarehe 07 Oktoba 2021. Wateule wote wataapishwa tarehe 11 Oktoba, 2021 saa 5:00 Asubuhi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

error: Content is protected !!