Kiungo wa kati wa Juventus Adrien Rabiot (26) anahusishwa kuwa moja ya wachezaji wanaowindwa na Newcastle United, taarifa kutoka Juventus zinasema kwamba wapo tayari kumuuza mchezaji huyo dirisha dogo la usajili mwezi januari ili kuwasaidia kupata fedha za kumsajili kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni au Donny van de Beek kutoka Manchester United. (Calciomercato).
Klabu ya Arsenal inajiandaa kutuma ofa ya euro milioni 30 kwa ajili ya usajili wa winga wa Club Bruges Noa Lang, 22 (Voetbal24).
Klabu ya Monaco imetangaza kuwa mchezaji wao Aurelien Tchouameni (21) anapatikana kwa dau la euro milioni 60. Mchezaji huyo anayatiwa na klabu za Real Madrid, Manchester City, Chelsea na Liverpool (Marca).
Klabu ya Barcelona ipo kwenye mazungumzo ya awali na kiungo wa Hispania Pedri (18) juu ya mkataba mpya na ambapo mchezaji huyo yupo tayari kusaini mkataba ambao utaendelea hadi mwaka 2026 huku mkataba huo ukiwa na kifungu cha kutolewa cha zaidi ya euro milioni 600 (Goal).
Pia Barcelona imepania kuachana na Philipe Coutinho 29, katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari na Liverpool wako wazi kumrudisha mchezaji huyo kunako Anfield (El Chiringuito TV – Express).
> Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 13 (Chamberlain mbioni kurudi Arsenal, Man City ikimnyatia Haaland)
Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers ni mmoja wa kocha anayepewa nafasi kubwa kuinoa klabu ya Newcastle United iwapo wamiliki wapya wa klabu hiyo wataamua kumtimua kocha wa sasa Steve Bruce (Sky Italy via Mirror).
Kocha wa Watford Claudio Ranieri (69) anasema anaweza kuvunja rekodi ya Roy Hodgson kama kocha mkongwe wa Ligi Kuu ya England (Mirror).
Klabu ya Real Madrid imeonyesha nia ya kumsajili beki wa Chelsea Antonio Rudiger (28). Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na klabu yake hiyo ya London ambapo mkataba wake unaelekea ukingoni mwisho wa msimu huu (Marca – Spanish).
Beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Mats Hummels 32, amemuonya Erling Haaland 21, huenda asipate “malisho mazuri” atakapoondoka klabuni hapo. Klabu za Manchester City, Manchester United, Chelsea na Real Madrid zinahusishwa kuwa na nia ya kumsajili fowadi huyo (Bild – German).
Phil Foden amesitisha mpango wake wa kusaini mkataba na Manchester City wenye thamani ya karibu pauni milioni 50, huku makubaliano ya kiungo huyo ya miaka sita yakimuwezesha kulipwa pauni 150,000 kila wiki (Mirror)
Manchester United inaweza kufufua juhudi zao za kumsajili beki wa kati wa Sevilla 22, Jules Kounde, ambaye pia anaendelea kuwa lengo la Chelsea (Fichajes – FourFourTwo).
Paris St-Germain inaweza ikamsajili mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic (21) kama mbadala wa Kylian Mbappe (22) ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu. PSG inakabiliwa na ushindani wa kumsajili mchezaji huyo wakimataifa wa Serbia kutoka kwa Tottenham, Juventus na Bayern Munich ambazo zote zinahusishwa na mchezaji huyo (Le 10 Sport – French).