Manufaa yatakayo patikana baada ya ushirikiano katika ya Serikali na Serikali ya Dubai.

HomeKitaifa

Manufaa yatakayo patikana baada ya ushirikiano katika ya Serikali na Serikali ya Dubai.

Yafuatayo ni manufaa ambayo yanatarajiwa kupatikana iwapo Bunge letu Tukufu litaridhia Azimio hili na kuwezesha Serikali kuendelea na hatua zinazofuata za majadiliano na Serikali ya Dubai. Baadhi ya manufaa yatakayopatikana ni pamoja na:

i. Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24. Hii itapunguza gharama za utumiaji wa Bandari yetu. Matokeo yake itaongeza idadi ya meli zitazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33;

ii. Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka siku 4.5 mpaka siku 2;

iii. Kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 kutokana na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA;

iv. Kupunguza gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje kwenda nchi za Jirani, kwa mfano kutoka US$ 12,000 mpaka kati ya US$6,000 na US$7,000 kwa kasha
linalokwenda nchi ya Malawi, Zambia au DRC. Hii italeta Watumiaji wengi kwenye Bandari ya Dar es Salaam;

v. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 158;

vi. Kuongezeka kwa Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya Forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi Trilioni 7.76 za mwaka 2021/22 hadi Shilingi Trilioni 26.7 za mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 244;

vii. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 mwaka 2021/22 hadi ajira 71,907 ifikapo mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 148;

viii. Maboresho ya maeneo ya kuhudumia shehena ya makasha na kuweka mitambo yenye Teknolojia ya kisasa;

ix. Kuendeleza eneo la kuhifadhia mizigo la Bandari Kavu kwa kuweka miundombinu ya kisasa ya kuhudumia aina zote za shehena;

x. Maboresho ya magati ya kuhudumia Majahazi na Abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitalii zitakazo ongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la Taifa;

xi. Kusimika Mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya shughuli za bandari na kuwaunganisha wadau wake;

xii. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer);

xiii. Uanzishwaji wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi/Viwanda; na

xiv. Kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi; kuchagiza shughuli za Viwanda na Biashara; kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; Watanzania kunufaika na teknolojia na ujuzi wa uendeshaji wa bandari kisasa; na kujenga mahusiano ya kidiplomasia.

error: Content is protected !!