Muliro: Kama yupo serious aripoti polisi

HomeKitaifa

Muliro: Kama yupo serious aripoti polisi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kama aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda anahitaji msaada ya kiusalama basi ni vyema afate utaratibu kwani anaujua.

Kamanda Muliro amesema yeye hajapokea malalamiko yoyote kuhusu kutishiwa amani kwa Makonda hivyo kumwambia kama anachosema kwenye mitandao ya kijamii ni kweli basi ni vyema akafata utaratibu uliopo wa kwenda kwenye kituo chochote cha polisi na kueleza shida zake.

“kama ana hofu ana ripoti kituo cha polisi kama ni kweli, mtu yoyote raia wa nchi hii ana haki ya kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili jambo lichunguzwe kama ni kweli lakini mimi hiyo taarifa sijaiona,

“sasa kama watu wanaacha vituo vya polisi… siwezi kukomenti, mimi najua watu ambao wako-serious wanaripoti mambo kwenye vituo vya polisi ,” alisema Kamanda Muliro.

Amejibu hayo baada ya Makonda kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu watu ambao wanahatarisha maisha yake na kutaja makundi ya watu watano.

error: Content is protected !!