Tetesi za soka Ulaya leo Septemba 24 (Ousmane Dembele kwenda Man United, Haaland kuondoka Dortmund)

HomeMichezo

Tetesi za soka Ulaya leo Septemba 24 (Ousmane Dembele kwenda Man United, Haaland kuondoka Dortmund)

Borussia Dortmund inaweza kuwasilisha ofa yao kupata huduma ya winga wa Juventus na Italia Federico Chiesa, 23, endapo klabu hiyo ya Bundesliga itampoteza mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, msimu ujao wa joto (Calciomercato – Italian)

Meneja wa Ureno Paulo Fonseca, 48, anasema hatua yake ya kuifundisha Tottenham ilitibuka kwa sababu mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici alitaka Spurs icheze mpira wa  ya kujilinda (Telegraph).

Manchester United wamefanya mawasiliano na Barcelona juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa 24 Ousmane Dembele (El Nacional, MEN).

Kiungo wa kati wa Real Madrid ya Uhispania Marco Asensio, 25, pia ni miongoni mwa wanaolengwa na Liverpool (Fichajes.Net, Sun).

Liverpool bado ipo mbioni kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa West Ham Jarrod Bowen. Walihusishwa na ofa ya pauni milioni 20 kwenye dirisha kubwa la usajili msimu huu (Liverpool Echo).

Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann anasema bado hajazungumza na mkurugenzi wa michezo Hasan Salihamidzic kuhusu Rudiger, ambaye hana mkataba wake unaisha msimu ujao (Eurosport).

error: Content is protected !!