Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 28 (Isco kutua Everton, Mata Kuondoka Man United)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Septemba 28 (Isco kutua Everton, Mata Kuondoka Man United)

West Ham ina mpango wa kumuuza Rice kwa dau la £90m ikijiandaa na dau la kumpata mrithi wake (Football Insider).

Meneja wa Everton Rafael Benitez anataka kuwasajili kiungo wa Hispania Isco, 29 na mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 23, Goodison Park wakitokea Real Madrid kwa mkataba mfupi wa mkopo mwezi Januari (Defensa Central – Spanish).

Barcelona bado ina nia ya kutaka kumsajili mlinzi wa Juventus na timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt (22) na iko tayari kumtoa golikipa wa Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen (29) na mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay (27) kama sehemu ya kukamilisha mpango huo (Calciomercato – Italian).

Mshambuliaji wa Club Brugge Noa Lang (22) yuko tayari kutua Arsenal lakini washika bunduki hao wa London wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan wanaomtaka pia mholanzi huyo (Voetbal24, Mirror).

Real Madrid wanafikiria kupeleka ofa kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Hispania Pedro Porro (22) ambaye yupo kwa mkopo Sporting Lisbon akitokea klabu ya Manchester City (O Jogo – Portuguese).

Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vya England vinavyotajwa kumfuatilia kiungo wa Ivory Coast Franck Kessie (24) ambaye amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya AC Milan (90min).

Manchester United imeamua kuelekeza nguvu zake kwa kiungo wa Leeds United Kalvin Phillips, 25, baada ya kuachana na mipango yao ya kumsajili kiungo mwenzake wa England Declan Rice, 22, kutoka West Ham (Star).

Crystal Palace wanamfuatilia kwa karibu Tom Davies, 23 wa Everton kufuatia hali ya sintofahamu ya mustakabali wa kiungo huyo wa England (Football Insider).

Barcelona inahitaji kumsajili kiungo wa Sweden, Williot Swedberg (17) kutoka Hammarby (Expressen – Swedish).

Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema Real Madrid ni klabu “inayomshawishi” Erling Haaland (21) wakati mshambuliaji huyo wa Norway akiangalia mustakabali wake wa baadae (AS – Spanish).

Vilabu vya Dortmund na Hoffenheim vinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa England kutoka West Bromwich Albion mwenye umri wa miaka 17 Reyes Cleary (Mail).

Jacob Ramsey, kiungo kinda wa Aston Villa (19) anaripotiwa kutakiwa na Manchester City, huku mabingwa hao wa ligi kuu England wakimfuatilia kwa karibu Muingereza huyo (Fichajes – Spanish).

Kiungo wa zamani wa Hispania Juan Mata (33) anaangalia mustakabali wake kufuatia kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara Manchester United msimu huu (Manchester Evening News).

Kiungo wa Roma Steven Nzonzi anakaribia kutua klabu ya Al Rayyan ya Qatari ambapo dirisha la usajili huko linafungwa Septemba 30 na mkataba wa kiungo huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 32 unamalizika mwaka 2022. (Calciomercato – in Italian)

error: Content is protected !!