Tony Blair: Rais Samia anapambana kuleta maendeleo kwa wananchi

HomeKitaifa

Tony Blair: Rais Samia anapambana kuleta maendeleo kwa wananchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe Tony Blair, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) amemshukuru na kumhakikishia Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitihada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.
Aidha, Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

error: Content is protected !!