Tovuti kadhaa za wizara muhimu nchini Kenya zimevamiwa na shambulio la kimtandao leo asubuhi, hali iliyosababisha kukosekana kwa huduma kwa muda.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, wadukuzi walibadili muonekano wa kurasa hizo, wakafuta taarifa halali na kuweka maandishi yasiyoidhinishwa kama “Access denied by PCP”, “We will rise again”, “White power worldwide” na “14:88 Heil Hitler”.
Wizara zilizolengwa ni pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani, Afya, Elimu, Nishati, Kazi na Maji.
Shambulio hilo limesababisha hitilafu katika upatikanaji wa huduma muhimu za Serikali na kuzua usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaotegemea mifumo hiyo.



