TRA yakusanya asilimia 103.9 ya lengo la makusanyo kwa kipindi cha Julai 2024 – Juni 2025

HomeKitaifa

TRA yakusanya asilimia 103.9 ya lengo la makusanyo kwa kipindi cha Julai 2024 – Juni 2025

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 (Julai 2024 – Juni 2025 ) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 32.26, sawa na asilimia 103.9 ya lengo la Shilingi Trilioni 31.05.

Aidha, katika robo ya nne ya pekee (Aprili-Juni 2025), TRA imekusanya Shilingi Trilioni 8.22, sawa na ufanisi wa asilimia 104.8, dhidi ya lengo la Shilingi Trilioni 7.84. Hii ni ongezeko la asilimia 15.8 kutoka makusanyo ya Shilingi Trilioni 7.09 ya kipindi kama hicho mwaka 2023/24.

Mafanikio hayo yamechangiwa na ushirikiano imara wa TRA na walipa kodi, utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu, kuimarika kwa ufanisi wa watumishi wa TRA na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na biashara.

Pamoja na hayo, katika mwaka wa fedha 2025/2026, TRA imelenga kukusanya Shilingi Trilioni 36.066.

error: Content is protected !!