Trilioni 1 zapatikana soko la madini Geita

HomeBiashara

Trilioni 1 zapatikana soko la madini Geita

Soko kuu la dhahabu mjini Geita limeingiza jumla ya shilingi trilioni 1.1 tangu kuanzishwa kwake mwa 2018.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa maonesho ya nne ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya madini, leo mjini Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemery Senyamule amesema fedha hizo zimepatikana baada ya kuuzwa kwa  kilo 10,780 za madini ya dhahabu.

Senyamule amesema mbali na uzalishaji huo pia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 yamewezesha kupatikana kwa zaidi ya shilingi bilioni 28.2 kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) katika fedha zinazotokana na uwajibikaji wa makampuni kwa jamii ambazo zimewezesha mabadiliko makubwa katika miundombinu ya afya na elimu.

Pamoja na mafanikio hayo, pia imeelezwa kwamba sekta ya madini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa miundombinu unaofanywa na wachimbaji wadogo. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa wachimbaji hao.

Maonesho ya  nne ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini yanafanyika mkoani Geita huku kukiwa na washiriki 481 kutoka Tanzania na nchi nyingine kama Rwanda, Dubai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, India na Uganda.

error: Content is protected !!