Trump akabidhiwa mkanda wa mapigano

HomeKimataifa

Trump akabidhiwa mkanda wa mapigano

Rais aliyepita wa Marekani Donald Trump ametunukiwa mkanda wa heshima. Rais Donald Trump amekabidhiwa mkanda mweusi na taasisi na Chuo cha Taekwondo cha Korea Korea Kusini kutokana na mahaba na mapenzi yake juu ya mchezo huo.

Mkanda huo ulitolewa kwa Trump siku ya Ijumaa na Lee Dong-seop, Rais na kiongozi wa makao makuu ya Taekwondo duniani kilichopo Seoul nchini Korea. Ghafla hiyo fupi imefanyika katika makazi binafsi ya Trump katika visiwa vya Mar-a-Lago Florida.

Trump alitamka kuwa amefurahi sana kupokea mkanda huo, na amesema pia atakuwa anauvaa mkanda huo na nguo zake za Taekwondo katika Bunge la Marekani kama atarudi tena White House huko mbele ya safari.

Kwa mujibu ya tovuti ya Taekwondo ya nchini Korea Kusini, ili uwe mkufunzi wa mchezo huo angalia usomee kwa miaka 9 kisha uwasilishe andiko lisilopungua kurasa 10 kueleza maisha na uzoefu wako kuhusu Taekwondo.

error: Content is protected !!