Viashiria vinavyoonesha uchumi wa Tanzania umezidi kuimarika
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetangaza mwenendo wa viashiria vya kiuchumi vya muda mfupi kati ya Januari-Juni mwaka huu, ambavyo vimeonesha kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika.
Kiashiria cha kwanza kilichotazamwa ni kuongezeka kwa Idadi ya utalii. Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Daniel Masolwa amesema idadi ya watalii waliongia nchini katika kipindi cha Januari hadi Juni inanonesha kuimarika kwa sekta ya utalii.
Kiashiria kingine kwa mujibu wa NBS ni uzalishaji wa saruji ambao umezidi kuimarika sana. Kuhusu huduma za mawasiliano, NBS imesema kumekuwa na ongezeko kubwa, kutoka dakika za kuzungumza bilioni 31.3 katika kipindi cha Januari-Juni 2019 hadi dakika bilioni 42.9 katika kipindi kama hicho mwaka huu.
Uzalishaji wa umeme, takwimu zinaonesha umeongezeka kutoka kilowati milioni 3,478 katika kipindi cha Januari – Juni 2018 hadi kilowati 4,053 katika kipindi kama hicho mwaka huu.
Mkurugenzi wa Sensa za Takwimu za Jamii, Ruth Minja amesema mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti umebaki 3.8% kama ulivyokuwa mwezi Julai.