Applications 7 muhimu kuwa nazo kwenye simu

HomeElimu

Applications 7 muhimu kuwa nazo kwenye simu

 

1. Word Lens
Kazi hii ya application ni kutoa tafsiri ya maneno mbalimbali kwa kuyapiga picha. Ukifika katika eneo ambalo hujui lugha ya hapo, au kupata maana ya maelekezo fulani kwenye bango, unaweza kutumia application hii kupata maana na ikawa msaada mkubwa kwako. Application hii unaweza kusomea hata gazeti.

2. Think Tracker
Application hii itakujuza ni nani ameshika au kuchezea simu yako. Mtu akijaribu kufungua simu yako na kukosea nywila mara 3, kwa kutumia camera ya mbele simu hii inampiga picha mtu huyo, kisha picha zile kutumwa kwenye barua pepe yako (email) na kuhifadhiwa huko.

3. SpineMe Alarm Clock
Application ni kwa wale watu wavivu kuamka asubuhi, au wale ambao wanaendelea kulala hata kama alarm waliyoweka imelia. Application hii itakufanya usirudi tena kulala kwani haitonyamaza hadi uamke na kuanza kutembea.

4. Photmath
Inakuonesha hatua zote za kukokotoa hesabu hadi kuendea jibu. Kutumia application hii kutakufanya uwe na uwezo wa kujifunza hesabu kwa njia rahisi kabisa. App hii inafanya hesabu yoyote ile, unachotakiwa kufanya ni kuelekeza camera yako kwenye swali na uiache ifanye kazi yake.

5. Clap to find
Kuna muda simu yako imeiweka silent (kimya) na unaweza kupata shida kuiona. Kwa kutumia application ya clap mode unaweza kupiga makofi machache na simu yako itaita hata kama uliiweka silent.

6. Tasker
Application inakusaidia kufanya mambo kadhaa bila hata wewe kugusa simu yako. Inaweza kuzima intaneti kwenye simu yako ukiwa umelala usiku. Inaweza kutuma meseji yenyewe kwa mtu anayekupiga kama ukiwa kwenye kikao au umetingwa na kazi au kuanza kupiga muziki pale tu utakapochomeka earphones.

7. Skye Real-time Language Translator
Hii inafanya kazi kama mkalimani, unaweza kuzungumza kwa lugha yako na mtu, na mtu unayezungumza nae atakusikia kwa lugha yake, ina lugha 40.

error: Content is protected !!