Manara; Nilisema uongo, niko tayari kwenda gerezani

HomeMichezo

Manara; Nilisema uongo, niko tayari kwenda gerezani

Msemaji wa timu ya soka ya Yanga, Haji Sunday Manara amesema yeye hakuwahi kuwa (shabiki) wa Simba. Amesema amekuwa Yanga katika maisha yake yote.

Akihojiwa katika kipindi cha Sporst HQ kinachoruka kupitia kituo cha redio cha EFM leo hii, Haji alikwenda mbali kwa kusema yuko tayari kuhukumiwa kwenda gerezani, kwani maneno yake ya kuonesha kwamba Simba ni timu kubwa, yalikuwa uongo mtupu. Haji amesema anajutia kufanya kosa hilo, kwa kuwadanganya Watanzania.

Haji Manara alikuwa msemaji wa Simba kwa takribani miaka sita kabla ya kujiunga na Yanga mwaka huu.

error: Content is protected !!