Uhusiano wa Tanzania na China ni endelevu

HomeKitaifa

Uhusiano wa Tanzania na China ni endelevu

Rais Samia Suluhu amekutana na kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

Mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya China na Tanzania. Tanzania ni nchi ambayo Rais Xi aliweka kwa mara ya kwanza sera ya China kwa Afrika katika enzi mpya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na ujumbe wake katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

Wakati wa ziara yake ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 2013, Rais Xi aliweka wazi kanuni za ukweli, matokeo halisi, urafiki na nia njema—vipengele vikuu vya sera ya China kuelekea Afrika. Kanuni hizi pia zinaakisi mpango muhimu unaoonyesha maoni ya pamoja ya nchi za Kusini mwa Dunia juu ya jinsi ya kufanikisha maendeleo kupitia juhudi za pamoja.

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

Rais Xi alieleza utayari wa China kuendeleza zaidi uhusiano wake na Tanzania ili kutoa mfano bora wa mahusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano kati ya mataifa ya Kusini mwa Dunia.

error: Content is protected !!