Uingereza yakubali vyeti vya chanjo ya UVIKO-19 kutoka Tanzania

HomeKimataifa

Uingereza yakubali vyeti vya chanjo ya UVIKO-19 kutoka Tanzania

Octoba 7, 2021 Serikali ya Uingereza kupita Ubalozi wake nchini Tanzania ulitoa tamko la kupunguza vikwazo vya kuingia Uingereza kwa watanzania na waingereza waishio Tanzania. Awali Serikali ya Uingereza ilieleza furaha yaka kwa kuiondoa Tanzania miongoni mwa mataifa hatari kusafiri kutokana na ugonjwa wa UVIKO – 19.

Oktoba 29, 2021 Serikali ya Uingereza imetamka tena kuwa kuanzia Novemba 1, 2021 Serikali ya Uingereza itaanza kutambua vyeti vya chanjo ya UVIKO-19 vinavyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hii itasaidia watu waliochanjwa kutoka Tanzania kutokuwa na sharti la kukaa karantini wala kutengwa pindi wanapowasili Uingereza. Hatua hii itategema tu endapo mtu amechanjwa moja ya chanjo zinazotambulika na Serikali ya Uingereza.

error: Content is protected !!