Ummy: Serikali itakarabati Uwanja wa Mkwakwani

HomeKimataifa

Ummy: Serikali itakarabati Uwanja wa Mkwakwani

Mbunge wa Tanga Ummy Mwalimu amesema atashirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kukarabati uwanja wa Mkwakwani uliofungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kutumika katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Waziri Ummy amesema wakati akifungua tawi la Coastal Union – Oddo Ummy jijini Tanga kuwa atashirikiana na wamiliki ambao ni CCM kukarabati na kufunga taa ili uweze kutumika katika michezo mingi ikiwemo ile ya usiku.

Uwanja huo una changamoto ya ubovu sehemu za kuchezea, vyoo na vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji na waamuzi.

“Najua hamtaona michezo hii ya mwanzo, lakini niwaahidi kwamba uwanja tunaukarabati na tutauwekea taa ili michezo mingine ifanyike usiku,” alisema Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya.

error: Content is protected !!