Umri wa kuishi kwa wanawake Tanzania umeongezeka hadi miaka 70

HomeKitaifa

Umri wa kuishi kwa wanawake Tanzania umeongezeka hadi miaka 70

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imeripoti kuwa wastani wa umri wa kuishi kwa mwanamke wa Kitanzania anayezaliwa mwaka 2025 umeongezeka hadi miaka 70, kutoka miaka 69 mwaka 2022. Kwa sasa, wanawake nchini wanakadiriwa kufikia 34.7 milioni, sawa na asilimia 50.96 ya watu wote.
 
Takwimu zinaonyesha pia kuwa asilimia 25.8 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wanamiliki ardhi. Katika uongozi, wanawake wana nafasi mbalimbali: mawaziri (29.2%), wabunge (37.4%), wakurugenzi wa halmashauri (30.9%), wakuu wa mikoa (29.9%) na wakuu wa wilaya (28.89%).
 
Aidha, wanawake wenye ulemavu ni chini ya asilimia 11.6 ya wanawake wote nchini.
error: Content is protected !!