Ushauri wa Kinana kuhusu trafiki waanza kufanyiwa kazi

HomeKitaifa

Ushauri wa Kinana kuhusu trafiki waanza kufanyiwa kazi

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kwamba tayari umeanza kufanyia kazi ushauri uliotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapunduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana jana tarehe 28.07.2022 kuhusu kupunguza askari wa trafiki mjini.

Jeshi hilo limesema limeanza kuweka mikakati mizuri ya kutekeleza ushauri huo ambao pia umepokelewa kwa maoni mengi kutoka kwa wananchi.

Aidha, Jeshi la Polisi limeweka wazi utayari wake wa kufanya kazi bega kwa bega na wadau mbalimbali panoja na kupokea maoni, ushauri na malalamiko na kufanyia kazi kwa wakati ili kuboresha utendaji wake na kuwaondolea kero wananchi.

error: Content is protected !!