Ushirikiano kati ya Tanzania na Japan wazidi kuimarika

HomeKimataifa

Ushirikiano kati ya Tanzania na Japan wazidi kuimarika

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano wa Tanzania na Japan umezidi kukua na kuimarika katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia ambapo mauzo ya biashara kati ya nchi hizo yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni saba mwaka 2023 hadi Dola bilioni 37 kwa mwaka 2024.

Amesema hayo jana alipomwakilisha Rais Samia Suluhu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan.

Alisema Wajapan wanapenda sana bidhaa kutoka Tanzania zikiwemo za kilimo kama chai, kahawa, ufuta, tumbaku, tingatinga, vinyago, katani, viungo kama karafuu pamoja na madini yanayopatikana nchini.

Aidha, Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan na duniani kote waje kuwekeza katika maeneo kama elimu, afya, miundombinu, nishati, kilimo, utalii kwani Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na pia ina amani na utulivu.

 

error: Content is protected !!