Utakayoulizwa na karani wa sensa

HomeKitaifa

Utakayoulizwa na karani wa sensa

Mbali na kutaja idadi ya wanakaya, karani wa sensa atauliza kama una/ ana matatizo ya kukumbuka au kufanya kitu kwa umakini. Swali hili linataka kujua iwapo mhojiwa ana tatizo mojawapo kati ya haya mawili au yote. Majibu ya swali hili yataiswezesha serikali kujua idadi kamili ya watu wenye matatizo ya kumbukumbu na kupanga mipango ya kuwasaidia.

Pia mhojiwa ataulizwa iwapo yeye au kwenye kaya yake kuna mtu ana matatizo ya kujihudumia kama vile kuoga au kuvaa nguo.

Swali hili linalenga kujua watu wenye matatizo hayo na majibu yataiwezesha Serikali kujua idadi ya watu wenye tatizo la ulemavu wa mikono.

Swali jingine litakaloulizwa na karani wa sensa ni kama mtu ana matatizo ya kuwasiliana kwa kutumia ligha ya kawaida. Kwa mfano kuelewa au kueleweka na lengo ni kujua kama mtu ana matatizo hayo.

Sensa ya watu na Makazi itafanyika Agosti 23 mwaka huu ikiwa ni tukio la kihistoria lililobea mustakabali wa maendeleo ya kijamii. Kiuchumi na kiutamaduni kwa taifa.

error: Content is protected !!