Bashungwa ashtukia upigaji wa fedha Kilosa

HomeKitaifa

Bashungwa ashtukia upigaji wa fedha Kilosa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ameagiza uchunguzi wa haraka wa madai ya ubadhilifu wa Sh bilioni 1 za mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Prof Kabudi zilizotolewa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tamisemi inasema kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule 15 zilizopata Sh bilioni 1 kwa ajili ya kujenga shule ya Sekondari za Kidato cha Tano na Sita kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R), hata hivyo halmashauri hiyo haijakamilisha.

“Shule za maeneo mengine zilizopata fedha kama hizo zimekamilisha ujenzi lakini katika shule hii ni tofauti shule haijakamilika na fedha zimeisha hivyo nataka taarifa ya uchunguzi,” amesema Bashungwa na kuongeza.

“Sioni uhalisia wa gharama za ujenzi zimekua juu sana kuanzia kwenye ujenzi madarasa, mabweni, nyumba za walimu hazijakamilika sasa nataka timu maalum ije kuangalia thamani ya fedha zilizotumika.”

error: Content is protected !!