Utata watanda ripoti mpya juu ya chanzo cha UVIKO-19

HomeKimataifa

Utata watanda ripoti mpya juu ya chanzo cha UVIKO-19

Idara za usalama nchini Marekani zimeonekana kushindwa kueleza kuhusu chanzo halisi cha UVIKO-19 na kuachia ripoti yenye mkanganyiko kueleza makisio juu ya ugonjwa huo. Ripoti iliyotolewa inaonesha dhahiri kuwa bado haijulikani hasa ni nini chanzo cha UVIKO-19.

Ripoti imeeleza kuwa ugonjwa huo pengine umevuja kutoka kwenye maabara fulani au umetokea kwa njia ya asili tu.Ingawa wataalamu wengi wanakubaliana kuwa UVIKO-19 sio silaha ya kibaiolojia kama idhaniwavyo na wengi, lakini wataalam haohao wanahimiza uharaka wa uchunguzi juu ya chanzo cha ugonjwa kwani inaweza kuja kusumbua zaidi kukusanya taarifa muda ukipita sana.Ripoti hiyo imepokelewa kinyume kabisa na serikali ya China ikiweka wazi kuwa imekosa utashi wa kisayansi.

Ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Marekani inaeleza kuwa bado idara kubwa za usalama duniani zinapishana juu ya chanzo halisi cha UVIKO-19. Ingawa idara zote zinaamini katika nadharia kuu mbili juu ya chanzo cha ugonjwa huu, nazo ni, UVIKO-19 ni ajali ya kitafiti iliyotokea maabara na ni ugonjwa wa asili ulioanza kusambazwa na mnyama.

Rais Joe Biden wa Marekani ametoa neno baada ya ripoti hiyo kuchapishwa, ameishutumu serikali China kutotoa ushirikiano katika uchunguzi juu ya asili ya ugonjwa huo.“Taarifa za kina juu ya chanzo cha ugonjwa huu zimo miongoni mwa watu wa China, lakini tangu mwanzo serikali ya China imekuwa kikwazo kwa watafiti wa kimataifa kupata kibali kuruhusu uchunguzi wa ugonjwa huo.

Dunia inahitaji majibu, na haitakaa kimya hadi yapatikane,” amesema Biden. UVIKO-19 imeanzia China na hadi sasa watu milioni 4.5 wamepoteza maisha.

Timu ya Shirika la Afya Duniani ilizuru Wuhan, China na kuja na majibu kwamba pengine UVIKO-19 imeanza kusambaa kutoka kwa wanyama wanaouzwa sokoni, majibu hayo yamepigwa na wanasayansi wengi duniani.Biden ameagiza Idara za Usalama kutafuta taarifa juu ya ugonjwa huo na kutoa ripoti ambayo itakayoweka karibu na kuujua ukweli dhahiri juu ya ugonjwa wa UVIKO-19.

error: Content is protected !!