Utatoa faini mifuko 5 ya simenti ukivaa kimini au mlegezo

HomeKitaifa

Utatoa faini mifuko 5 ya simenti ukivaa kimini au mlegezo

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, viongozi wa kata ya Tandala, wilayani Makate Mkoa wa Njombe wametunga sheria ndogo za kuwakamata wananwake wanaovaa nguo fupi zinazochora maumbile yao pamoja na wanaume wanaovaa suruali chini ya makalio na kuwapiga faini ya mifuko mitano ya saruji itakayojenga miradi ya kata.

Maximilian Msigwa, Mtendaji wa Kata hiyo alisema uamuzi huo umefanyika ili kudhibiti mavazi yasifaa katika jamii na baadhi ya watu wameshakamatwa.

“Tumekuwa na mabinti wengi wanaokuja kutafuta riziki kwa njia tofauti, sasa wanapokosea ni lazima tuwanyooshe warudi kwenye mstari,akikamatwa analipishwa mifuko ya sarujo kwa ajili ya ujenzi kwa sababu tuna ujenzi wa shule yetu ya msingi Tandala,” alisema Msigwa.

Aidha, kabla ya sheria hiyo kuanza kufanya kazi, viongozi wa Kata iliwapa taarifa wamiliki wa kumbi za starehe na wananchi kwa ajili ya kujirekebisha kabla sheria hiyo haijaanza kufanya kazi.

error: Content is protected !!