Aliyekuwa mgombea ubunge wa Masasi Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2020, Mustapha Swalehe amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kuwa amefurahishwa na kasi ya maendeleo inayofanywa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu.
Swalehe alitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo, Geofrey Mwambe kwa kushirikiana na Mwenyekiti CCM Wilaya ya Masasi, Mariam Kasembe na Katibu wa chama hicho, Dodas Zimbihile.
Alisema alikuwa ndani ya CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20 lakini kwa sasa anaridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Samia.
“Leo nimeamua kujiunga na CCM na sasa mimi ni mwanachama mpya, kazi iliyofanywa na mbunge wetu kuleta maendeleo inastahili kuungwa mkono,” alisema.
Kwa mujibu wa Swalehe, kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu bali pale unapoona maendeleo yanayofanywa kuna kula sababy ya kuunga mkono maendeleo hayo na sio kuendelea kupinga.