Uwanja wa Mkapa kufungwa kwa mwezi mmoja

HomeMichezo

Uwanja wa Mkapa kufungwa kwa mwezi mmoja

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeshauri Uwanja wa Benjamini Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam kutotumika kwenye mechi zao kwa kile kilichoelezwa umeharibika eneo la kuchezea (pitch) na sasa utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho.

Hivyo, baada ya mechi ya leo Jumatano ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na KMC, itakayochezwa kuanzia saa 1:00 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa, uwanja huo unapaswa kutumika mara tatu kwa wiki lakini hadi leo itakuwa ni mara ya nne kinyume na matumizi ya uwanja huo ambao hata kabla ya hapo ulilalamikiwa kutokuwa katika hali nzuri hasa eneo la kuchezea (pitch), kwani matumizi yamekuwa makubwa.

Meneja wa Uwanja huo, Salum Mtumbuka alisema baada ya mechi za CAF zilizochezwa wikiendi iliyopita walikutana na maofisa hao ambao waliwapa maelekezo namna ya kufanya marekebisho hasa eneo la kuchezea.

“Tulikubaliana kwa pamoja na Caf wakati marekebisho yanaendelea ambayo yatachukua muda wa mwezi mmoja, mechi zitakazochezwa hapo hapo labda zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa, mechi zingine za ligi kuu wanaotumia uwanja huu watatafuta viwanja vingine hata Uhuru upo.

“Simba na Yanga ndiyo wanaotumia huu uwanja kama uwanja wao wa nyumbani, ila ndani ya kipindi cha maekebisho haya hawatatumia mechi zao za Ligi Kuu kwenye uwanja huu, tunawapa Uwanja wa Uhuru ama watakavyoona wao,” alisema Mtumbuka.

 

error: Content is protected !!