Vanesa Mdee, Diamond kwenye tuzo moja na Beyonce

HomeBurudani

Vanesa Mdee, Diamond kwenye tuzo moja na Beyonce

Pamoja na Mwanadada Vanessa Mdee kuachana kabisa na mambo ya mziki na kuamua kufanya mambo mengine,ametwaja kuwania tuzo kubwa za muziki kutokea Uingereza zinazojulikana kama Urban Music Awards. Katika tuzo hizo Vanessa anagombania kipengele cha Mwanzamuziki wa mwaka kutoka Afrika pamoja na msanii mwingine kutoka Tanzania Nasseb Abdul maarufu kama Diamond.

Kipengele hiko cha msanii wa mwaka kutoka Afrika kinawaniwa na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali, Wasanii hao ni pamoja na Tiwasavage, Wizkid,Olakira, Davido,Burna Boy, Falz, Joe Boy na Rema wote kutokea nchini Nigeria, Darina Victry kutokea Cameroon, Fally Ipupa kutokea DRC, Sarkodie na Shatta Wale kutokea Ghana.

Tuzo za Urban Music Award ni tuzo namba moja duniani kwa muziki wa aina ya R&B, HipHop, Soul and Dance. Tuzo hizo zilianzishwa miaka 18 iliopita znafanyika katika mataifa mabalimbali lakini pia zinawaniwa na mastaa mbalimbali  kama Beyonce, Cardi B, Kanye west na wengine wengi.

error: Content is protected !!