Viumbe Ziwa Tanganyika wakadiriwa kupotea

HomeKitaifa

Viumbe Ziwa Tanganyika wakadiriwa kupotea

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi (Muungano na mazingira) nchini Tanzania Dr. Seleiman Jafo ametahadharisha upotevu wa viumbe washio katika ziwa Tanganyika.

Dr. Jafo amearifu kua, miongoni mwa viumbe elfu ishirini na mbili (22,000) wanaokadiriwa kupotea duniani, ni pamoja na wale washio katika ziwa hilo kubwa Barani Afrika.

Dr. Jafo aliyasema hayo katika mkutano wa kumi (10) wa nchi wanachama wa mkataba wa hifadhi na usimamizi endelevu wa ziwa Tanganyika uliofanyika huko Jijini Bujumbura Nchini Burundi na kusisitiza juu ya kuungana kwa pamoja na kujadili namna bora za kulilinda ziwa Tanganyika.

“Waheshimiwa mawaziri, mazingira tunayoishi yanabadilika kwa haraka sana na shughuli za binadamu zinatumia maliasili za dunia kwa kasi ya kutisha na kuharibu mifumo ya ikolojia.” Alisema Dr Jafo.

Katika mkutano huo, Serikali ya Tanzania walikabidhi uenyekiti wa umoja wa mkataba huo kwa burudi mara baada ya Tanzania kumaliza kutumikia muda wake wa uwenyekiti kwa mwaka mmoja.

error: Content is protected !!