Viwanda kutoa ajira milioni 6 kwa vijana

HomeKitaifa

Viwanda kutoa ajira milioni 6 kwa vijana

Serikali imetangaza kufungua fursa za ajira kwa vijana kupitia uwekezaji katika Sekta ya Viwanda na biashara, ikilenga kuanzisha na kuendeleza viwanda zaidi ya 9,000 vitakavyotoa ajira milioni sita ndani ya miaka sita ijayo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam jana, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, alisema mageuzi makubwa ya sera, sheria na mifumo ya biashara yameweka msingi imara wa kukuza uchumi wa viwanda, kuongeza thamani ya rasilimali, kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi.
 
“Tanzania ya viwanda haiwezi kujengwa bila vijana. Serikali imeweka misingi, imefungua masoko na imerahisisha mikopo. Sasa ni jukumu la vijana kuchukua hatua,”alisema.
 
Judith alisema kati ya mwaka 2021 hadi 2024, serikali imefanya marekebisho zaidi ya sheria mama 12 na sera muhimu ikiwemo Sera ya Taifa ya Biashara, Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda, Sera ya Uendelezaji wa Wajasiriamali Wadogo na Kati (SMEs), hatua iliyochangia kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara.
 
error: Content is protected !!