Kizz Daniel: Kweli begi langu moja lilisahaulika Nairobi

HomeBurudani

Kizz Daniel: Kweli begi langu moja lilisahaulika Nairobi

Msanii wa nchini Nigeria, Daniel Anidugbe maarufu Kizz Daniel  amewaomba radhi Watanzania kwa kushindwa kufanya onyesho lake mkoani Dar es Salaam.

Onyesho hilo lilipangwa kufanyika Jumapili Agosti 7,2022 lakini ilishindikana, lakini  imepangwa kurudiwa  Ijumaa Agosti 12,2022.

Akizungumza jana usiku Jumanne Agosti 9, 2022  na waandishi wa habari mkali huyo wa kibao cha Buga ameelezea sababu ya kutofanya onesho hilo ni  kusahau begi nchini Kenya.

“Nilisahau begi kama mlivyosikia wakati  wa safari yangu ya kuja huku na nilikuwa nimebaki na nguo nilizovaa ambazo ni kaptura na kobasi,” amesema.

Amesema baada ya jitihada mbalimbli za  kutafutiwa nguo alikuwa ameshakubali kupanda jukwaani saa  11 alfajiri  lakini kwa hali ilivyokuwa  ukumbini kwa muda huo  akaona kwa usalama waahirishe onyesho hilo.

“Nilikubali kwenda kwenye show lakini kwa kuwa muda ulikua umeenda na mashabiki walishaanza kufanya vurugu, nikashauriwa ni baki kwa sababu za usalama,” – amesema Kizz Daniel.

Amesema kutokana na lililotokea wamekubaliana na waliomleta kufanya onesho hilo Ijumaa  na itakuwa bure kwa wale waliokuwa wameshalipa fedha zao.

Amebainisha kuwa Tanzania ni nchi anayoipenda kwa kuwa imekuwa ikiupaisha muziki wake kwa kiasi kikubwa hata kuamua kuweka bendera ya Tanzania  kwenye video yake  na kukiri kujutia kilichotokea huku akiahidi hakitajirudia tena.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Str8up music, Sniper Montana ambao ndio wamemleta msanii huyo amesema waliolipia onesho mara ya kwanza hawatalipia tena na kuwataka walio na tiketi kuzihifadhi kwa ajili ya siku hiyo.

Montana amesema siku hiyo Kizz Daniel atapanda jukwaani kwa saa mbili mfulululizo.

Abel Ndaga, ofisa sanaa mwanadamizi wa  Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) amesema watahakikisha wanasimamia onesho hilo hadi kufanyika kwake.

Pia Ndaga aliwahakikishia wananchi kwamba kampuni iliyomleta msanii huyo ilifuata taratibu zote ikiwemo vibali na kutaka kuendelea kujenga imani nao.

“Hii kampuni  wamefanya kazi ya kuwaleta wasanii wa kimataifa kwa mwaka wa 12 sasa na hakujawahi tokea tatizo kama hilo. .

error: Content is protected !!