Vijana wanavyoinuliwa na Rais Samia kupitia vyuo vya ujuzi

HomeKimataifa

Vijana wanavyoinuliwa na Rais Samia kupitia vyuo vya ujuzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejizatiti katika kutoa elimu ujuzi na hivyo itaendelea kuwekeza katika elimu ya ufundi ikiwemo ujenzi wa Vyuo vya VETA katika kila wilaya na Mikoa.

Amesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mbarali kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya Mradi wa Kukuza Ujuzi (ESPJ).

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wanachi wa Mkoa wa Mbeya na hususan Wilaya ya Mbarali kuhakikisha wanakitumia chuo hicho kupata ujuzi kulingana na shughuli zao za kiuchumi.

“Serikali yenu imeamua kujenga vyuo vya aina hii karibu katika kila wilaya maeneo kadhaa Tanzania madhumuni makubwa ni kwamba vijana wetu ndio mtakaokuja kusoma hapa…na kitakachofundishwa ni kazi zenu ambazo zinawazunguka hapa hapa.” alisema Rais Samia.

Akimkaribisha Rais Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema ujenzi wa chuo hicho umefikia asilimia 95 na kwamba hadi kukamilika utatumia Shilingi Bilioni 2.7.

Ameongeza kuwa Chuo hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi wa kozi fupi wapatao 240 na mwezi Januari 2023 kudahili wanafunzi wa kozi za muda mrefu wapatao 500.

error: Content is protected !!