Wabunge waomba mshahara milioni 23

HomeKimataifa

Wabunge waomba mshahara milioni 23

Wabunge wa Kenya wameomba ongezeko la 62% ya mshahara wao ili kufikia shilingi milioni 1.15 ya Kenya sawa na milioni 23 za Kitanzania.

Wabunge hao ambao kwa sasa wanalipwa kati ya Ksh 621,250 na 710,000 ~ Tsh 12.3m na 14.2m wameomba pia ruzuku ya kununua magari ya milioni 2.5 za Kenya na kurudishiwa Ksh 400,000 kama posho ya nyumba.

Wamedai kuwa wao hawana tofauti na majaji wa Mahakama ya Rufaa ambao hulipwa Tsh 23m.

Kwa kawaida wabunge hao huondoka na Tsh 100043.03 kwa kila kikao cha kamati, huku mwenyekiti akiambulia Tsh 200086.06 na makamu mwenyekiti TSh150064.54. Wabunge wanataka marupurupu hayo yaongezwe hadi zaidi ya Tsh 150064.54 kwa mbunge wa kawaida.

Mei Mosi Rais wa Kenya alipandisha mishahara kwa atumishi kwa 12%.

 

error: Content is protected !!