Wadau waitwa kujadili nauli za SGR

HomeKitaifa

Wadau waitwa kujadili nauli za SGR

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeitisha kikao cha wadau kujadili nauli za abiria wa treni ya njia ya Reli ya Kisasa–SGR ambapo Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapendekeza Sh 59,494 na Sh71,392 kwa daraja la kwanza na la kati mtawalia kwa mtu mkubwa anaye safiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

TRC imependekeza nauli ya Sh 24,794 na Sh 29,752 kwa daraja la kawaida na kati kwa mtu mkubwa anaye safiri kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

Latra imesema inahitaji maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridia viwango vya nauli kwa huduma za treni hiyo. Mkutano huo umepangwa kufanyika Desemba 19, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Anatorglo.

error: Content is protected !!