Wafanyakazi 28 wa GGM kizimbani kwa uhujumu uchumi

HomeKitaifa

Wafanyakazi 28 wa GGM kizimbani kwa uhujumu uchumi

Wafanyakazi 28 wa Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu na udanganyifu.

Washtakiwa hao walisomewa mashitaka 29 wanayodaiwa kuyatenda kati ya Agosti 31, 2020 hadi Julai 6, 2021.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, James Palangyo akishirikiana na Dorcas Akyoo wamesema kuwa kwa nyakati tofauti kati ya tarehe tajwa walitenda makosa ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 107.5.

Kosa jingine linalowakabili ni wizi wakiwa waajiriwa, na kufanya udanganyifu unaohusisha madini kinyume na sheria.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo wamerejeshwa mahabusu hadi Septemba 23 shauri litakapotajwa tena.

error: Content is protected !!