Wapiga dili watorosha Kontena 400 Bandarini, mamlaka yashtuka

HomeKitaifa

Wapiga dili watorosha Kontena 400 Bandarini, mamlaka yashtuka

Kutokana na taarifa za awali zinadai kuwa zaidi ya Kontena 400 zimetoroshwa katika maeneo mbalimbali ya bandari kavu jijini Dar es Salaam, Kontena hizo zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye bandari kavu zikisubiria utaratibu wa forodha. Utoroshwaji huo unadaiwa kufanyika chini ya Kampuni moja inayoongozwa na mtanzania (jina lake limehifadhiwa) pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali.

Uchunguzi ulianza hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuvunja bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kutokana na kuwepo kwa madai ya ubadhirifu unaofanywa katika taasisi hiyo pamoja na kuitaka Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kufanya uchunguzi ili kubaini ufisadi wote uliofanyika.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia swala hilo kwani bado uchunguzi unaendelea katika bandari hiyo ya Dar es Salaam ili kubaini mtandao mzima wa hujuma hizo ili kuweza kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa watakaobainika.

Aidha kamishna huyo aliongezea kwa kusema kuwa kulingana na taarifa zilizopo ni kwamba kontena hizo 400 zilizotoroshwa hivi karibuni na wahusika hao, lakini TRA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari waliweza kugundua njama hizo na kuweza kuyakamata mitaani. Chanzo gazeti LAJIJI

error: Content is protected !!