Amuua kikatili na kisha kumla nyama

HomeKitaifa

Amuua kikatili na kisha kumla nyama

Mkazi wa Kitongoji cha Chang’ombe, Kijiji cha Kaloleni wilayani Songwe, Berta Shugha (69) ameuawa kikatili na mwili wake kukatwa vipande vipande huku baadhi ya viungo vikidaiwa kuliwa na muuaji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Alex Mukama, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari mtuhumiwa wa mauaji hayo ameshakamatwa.

Kamanda Mukama alimtaja mtu anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni Lazaro Adamson (40), mkazi wa Kaloleni ambaye anadaiwa kufanya mauaji hayo juzi.

Wakizungunzia tukio hilo, baadhi ya wakazi wa Chang’ombe walisema walishtukia kuwapo mauaji hayo baada ya kuona damu kwenye maeneo mengi ya nyumba ya mtuhumiwa, jambo ambalo halikuwa la kawaida.

Jesca Abraham ambaye ni jirani wa mtuhumiwa, alisema baada ya kuona damu kwenye makazi ya Lazaro, walihoji na kujibiwa na mtuhumiwa kuwa alikuwa amechinja mbuzi kwa ajili ya kitoweo chake na alishachemsha kwa ajili ya supu.

Jesca alisema kuwa baada ya kutoa taarifa polisi, askari walifika kwenye nyumba hiyo mara moja na kukuta baadhi ya viungo vya binadamu kisha kumkamata Lazaro na kuondoka naye.

error: Content is protected !!