Rais Samia aweka historia

HomeKitaifa

Rais Samia aweka historia

Kwa mara ya kwanza katika historia, benki za Tanzania zilipata faida ya jumla ya Sh. trilioni 1.16 mwaka 2022, huku zikisema faida hiyo inatokana na sera nzuri za biashara na uwekezaji zilizowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia aliwahi kusema wakati akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Oman lililofanyika Ikulu ya Oman kuwa serikali yake ni msimamizi tu lakini biashara zifanywe na seka binafsi kwa kuwa anaamini ndio chanzo cha ongezeko cha mapato nchini.

“Tangu nimeingia madarakani sera yangu imekuwa ni acha Serikali iwe msimamizi na sekta binafsi ifanye biashara, namaanisha kwamba hakuna tena biashara Serikalini, sekta binafsi itafanya biashara na Serikali sisi tunatengeneza mazingira rafiki kwa uwekezaji wa ndani au nje, hiyo ndiyo sera yangu,”

Pia alisema Tanzania “inatambua kazi kubwa” inayofanywa na wawekezaji katika kukuza uchumi na kutoa ajira “na ili kuchagiza uwekezaji wa ndani na wa nje tumejitahidi kuwa na sera Rafiki kwa uwekezaji na ufanyaji biashara.”

“Natambua kumekuwa na changamoto lakini nipo hapa na nawahakikishia nitakwenda kurekebisha chochote kilichowahi kutokea huko nyuma na tutakwenda kufanya kazi pamoja na kufanya uwekezaji kwa pande zote za nchi zetu,” amesema Rais Samia.

Kwa faida zilizopata benki za Tanzania, ni dhahiri kwamba Rais Samia Suluhu amefanikisha yale aliyoyaahidi kwa wawekezaji na sekta binafsi kwa ujumla.

error: Content is protected !!