Miswada mitatu yaridhiwa na Rais Samia

HomeKitaifa

Miswada mitatu yaridhiwa na Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia miswada mitatu kuwa sheria kamili na tayari zimeanza kutumika.

Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ambapo amesema miswada hiyo ni pamoja na mswada wa sheria ya Uwekezaji Tanzania wa mwaka 2023, Mswada wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi na mswada wa marekebisho wa sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2022.

Miswada hiyo iliyopitishwa katika mkutano wa 9 wa Bunge imepatiwa kibali na Rais Samia na sasa kuwa sheria kamili.

Spika Tulia amesema miswada hiyo sasa itatambulika kama sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka 2022, Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ya mwaka 2022 na sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali namba 3 ya mwaka 2022.

error: Content is protected !!