Mikataba ya Serikali kusainiwa Ofisi ya AG

HomeKitaifa

Mikataba ya Serikali kusainiwa Ofisi ya AG

Rais Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku Taasisi za serikali kuingia mikataba bila kushirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais Samia amesema hayo leo Alhamisi ya Septemba 29, 2022 akifungua mkutano wa kuanzishwa chama cha kitaaluma cha mawakili wa Serikali jijini Dodoma.

Amesema siku za nyuma mikataba ilisainiwa bila ofisi ya AG kufahamu na serikali kuingia hasara kubwa, wanapopata tatizo ndio wanaikumbuka ofisi hiyo huku waliosaini wamestaafu au wametangulia mbele ya haki hivyo hakuna wa kumuuliza.

Aidha, amesema mawakili wa serikali ‘jeshi kubwa’ linalotakiwa kulinda uchumi wa Tanzania kwa kutumiia kalamu zao.

“Nyinyi ni walinzi wa kalamu na siyo walinzi wa bunduki. Ni walinzi wa kalamu na sheria zenu. Kwa hiyo mwende mkalinde uchumi wetu, kwa haki na uadilifu ili nchi hii, iweze kupokea wawekezaji wengi zaidi, tuwekeze zaidi, tukuze uchumi masilahi yapatikane.”Amesema Rais Samia na kuongeza

“Nyinyi ndio ‘majeshi wa kulinda uchumi wetu, kisheria uchumi wetu lazima ulindwe, uwekezaji lazima ulindwe, biashara lazima zilindwe na walinzi wa hayo ni nyinyi.”Amesisitiza

error: Content is protected !!