Wajue Wayahudi wa Arusha

HomeKitaifa

Wajue Wayahudi wa Arusha

Taifa la Israel lipo karibu na nchi za Afrika Mashariki na nchi za kiarabu kuliko hata nchi nyingi duniani.

Kwa sababu ya ukaribu huu, Wayahudi wanaweza kusafiri kwenda Ethiopia, Zanzibar, Yemen na Tanzania Bara.

Na wayahudi wamefanya hivi kwa karne nyingi sana.Kabla ya mataifa ya Ulaya kuimarika kiuchumi miaka ya 1800s, kulikuwa na Wayahudi wa kutoka Yemen wajulikanao kama Yemenites na Wayahudi wa Oman wajulikanao kama Omanis katika nchi ya Tanganyika.

Mwaka 1942 Wayahudi 5000 kutoka Poland waliishi Arusha, wapo ambao walitoka Zanzibar kuingia Tanzania bara miaka 150 iliyopita kutafuta pembe za aina ya swala anayeitwa Kudu, wakati huo wanaofanya biashara hiyo kwa sana ni wayahudi kutoka Morocco na Yemen.Baada ya vita ya pili ya dunia, kuna waliorudi Israel, na wengine waliondoka punde tu baada ya Uhuru 1961.

Wale waliobaki wengi walikuwa ni wayahudi wa Ethiopia (Beta Israel).

Kuna waliofanikiwa kuoa na kuolewa na wayahudi wenzao, wengine wakaolewa na wamasai na hata kuchukua majina ya kiarabu.

error: Content is protected !!