Waliohudhuria mkutano ufunguzi wa bunge

HomeKitaifa

Waliohudhuria mkutano ufunguzi wa bunge

Wageni na wawakilishi wa mataifa mbalimbali wamehudhuria ufunguzi wa Bunge 13, linalozinduliwa na Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano Tanzania, Mussa Azzan Zungu Ijumaa Novemba 14,2025 amewataja wageni hao ndani ya Bunge kabla ya kumuita Dkt Samia kulihutubia na kulizindua.

Kwa mujibu wa Zungu, waliohudhuria ni pamoja na wawakilishi kutoka mataifa wageni kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo ya Marekani, China, Uswisi, Denmark, Uingereza.

Wengine wametoka mataifa ya Ufaransa, Japan, Urusi, Ubelgiji, Ireland, Finland, Norway, Jamaica, Poland, Ugiriki, Newzland, Romania.

error: Content is protected !!