Ratiba mazishi ya Mwai Kibaki

HomeKimataifa

Ratiba mazishi ya Mwai Kibaki

Mwili wa aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Kenya, Emilio Mwai Kibaki umewasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuagwa, leo mwili huo utaagwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, mawaziri, mabalozi, wakuu wa jeshi na viongozi wengine wakuu wa serikali.

Ratiba inasema wananchi wa Kenya watapata nafasi ya kuaga mwili wa Hayati Mwai Kibaki kesho Jumanne na Jumatano ndani ya majengo ya bunge la taifa.

Misa ya kitaifa ya kumuaga Hayati Kibaki itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 29 na kisha maziko kufanyika siku ya Jumamosi Aprili 30 nyumbani kwake huko Othaya Nyeri.

 

error: Content is protected !!