Waliokutwa na hatia ya kumiliki na kutumia bangi wasamehewa

HomeKimataifa

Waliokutwa na hatia ya kumiliki na kutumia bangi wasamehewa

Rais wa Marekani, Joe Biden amewasamehe watu wote waliokutwa na hatia ya kumiliki bangi.

Biden alitoa wito kwa majimbo ya Marekani kutekeleza hatua hiyo kuanzia Alhamis Oktoba 6.

Agizo hilo litanufaisha ‘’maelfu” ya watu, Ofisa Mkuu wa Utawala alisema.

Alichosema Biden: “Hakuna mtu anayepaswa kuwa gerezani kwa kutumia tu au kumiliki bangi.

“Kuna maelfu ya watu ambao wana hatia za awali za kumiliki bangi, ambao wanaweza kunyimwa ajira, nyumba, au fursa za elimu kama matokeo ya hukumu hizo,” alisema.

“Hatua yangu itasaidia kupunguza athari za dhamana zinazotokana na hatia hizi,” Biden alisisitiza.

error: Content is protected !!