Wanasiasa wapigwa marufuku kuongea makanisani

HomeKimataifa

Wanasiasa wapigwa marufuku kuongea makanisani

Askofu wa Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini Kenya Jackson Ole Sapit amepiga marufuku wanasiasa kuongea katika madhabahu ya kanisa hilo kote nchini Kenya.

Kiongozi wa upinzani toka chama cha ODM, Raila Odinga na Musalia Mudavadi wa chama cha ANC wamekuwa miongoni mwa waathiriwa wa kwanza wa agizo hilo ambapo katika ibada ya Jumapili walilazimika kukaa kimya katika sherehe ya kuapishwa kwa Askofu wa kwanza mwanamke wa kanisa hilo iliyofanyika Butere magharibi mwa Kenya.

Askofu wa Mkuu Jackson Ole Sapit ameeleza kuwa wanasiasa wamekiuka utakatifu wa asili wa madhabahu za makanisa. Nchini Kenya ni hali iliyozoeleka katika ibada za jumapili kwa wanasiasa kuzungumza huku wengi wakitumia nafasi hiyo kama viwanja vipya vya mikutano ya kisiasa kufuatia kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya kisiasa kutokana na COVID-19.

error: Content is protected !!