Orodha ya wasanii 10 tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa tovuti ya Classified.
1. Black Coffee – $60 milioni (TZS bilioni 139.1)
Jina lake halisi ni Nkosinathi Innocent Sizwe Maphumulo almaarufu kama Black Coffee. Ni mwanamuziki kutoka Afrika ya Kusini. Ni mwandazi wa muziki, DJ, anaimba pia na kuandika nyimbo. Black Coffee ameshinda tuzo kama BET, Best International Act, Best Deep House DJ. Pia anamiliki lebo ya muziki ya Soulistic Music ambayo ameitumia kutengeneza albamu zake zote tisa.
2. Wizkid – $21 Milioni (TZS bilioni 48.8)
Ni msanii wa pili kwa mkwanja mrefu barani Afrika. Kwa sasa ana deal kubwa sana ya ubalozi wa mtandao wa MTN ya Nigeria pamoja mtandao wa GLO ambapo mtandao huo umemlipa kiasi cha dola 240,000. Mwaka 2020 wizkid alipata ubalozi mkubwa na kampuni ya simu ya Tenco na pia ana deal kubwa nyingina na brand ya PUMA. Mwaka 2020 jarida maarufu la Forbes lilimtaja Wizkid kubwa na utajiri wa dola million 20 kama moja ya wasanii wenye mkwanja mrefu Nigeria.
3. Davido – $19 Milioni (TZSbilioni 44.04)
Davido amezaliwa Atlanta Marekani kutoka kwenye familia ya kishua ya Dr. Adedeji Adeleke. Utajiri wa Davido unatokana na muziki pamoja na dili kibao za ubalozi wa bidhaa mbalimbali. Show zake Davido huchaji kiasi kisichopungua dola 20,000 ndani ya Nigeria na 30,000 nje ya Nigeria. Utajiri wake pia unatokana na chanel yake ya youtube ambayo imetazamwa mara milioni 663 tangu ifunguliwe.
4. Don Jazzy – $18.5 milioni (TZS bilioni 42.9)
Jina lake huyu ni Collins Michael Ajereh, alizaliwa 1982. Jazzy ni msanii ukiachilia mbali mwandazi wa muziki. Anamiliki lebo maarufu ya muzika Afrika, Marvin Records. Jazzy ana mikataba ya pesa ndefu na makampuni kama MTN na Loyal Milk pamoja na V – Bank ya Nigeria.
5. Burna Boy – $17 milioni (TZS bilioni 39.4)
Burna ani rapper, mwandishi, anacheza pia ni msanii anayeimba vizuri sana, anatajwa kuwa kati ya wasanii bora sana wa kizazi chake. Ngoma yake ya kwanza 2012 ‘Like to Party’ kutoka kweny album yake ya L.I.F.E ambayo iliuza zaidi ya nakala 40,000 ndani ya siku moja. Burna anamiliki lebo ya muziki inayoitwa Spaceship Entertainment.
6. 2Face (2Baba – $16 milioni (TZS 37.1)
Jina lake ni Innocent Idibia, ni moja ya wasanii wakongwe wa kizazi hiki ambaye bado moto wake unawaka kwenye muziki. 2Face utajiri wake ni muziki pamoja na dili nono za ubalozi anazopata. Ameshinda tuzo nyingi kama MTV Music Awards, BET Awards.
7. Rude Boy – $16 milioni (TZS bilioni 37)
Moja ya wasanii wakubwa sana Nigeria na Afrika kwa ujumla. Alianza muziki akiwa na kaka yake Mr P ambapo kwa pamoja walijulikana kama P-Square. Rude Boy na kaka yake pamoja wameachia Album 6 ambazo 5 kati ya hizo zimeandaliwa kwenye rekodi yao.
8. Timaya – $12 milioni (TZS bilioni 27.8)
The Plantain Boy, ndivyo ambavyo mwanamuziki huyu mkubwa hujiita mara kwa mara. Alizaliwa 1980. Huyu ni Mfalme wa miondoko ya Dance Hall. Timaya anamiliki lebo ya muziki ya DM Records na label hii ndio imemlea msanii mkubwa kama Patoranking.
9. Olamide – $12 milioni (TZS bilioni 27.8)
Jina lake ni Olamide Adedeji Chose. Mtaani wanamjua kama Baddo kulingana na aina ya muziki anaoimba. Olamide amezaliwa 1989. Nyimbo zake anaimba kwa lugha ya Yoruba na imemfanya ajizolee mashabiki wengi sana magharibi mwa Nigeria hasa jijini Lagos. Olamide anamiliki Toyota Venza ($12,000), Range Rover Sports ($30,00), Mercedes – Benz G Wagon ($46,000), Range Rover Sports V8 ($168,000 – $180,000).
10. Mr. P – $11 milioni (TZS bilioni 25.5)
Mr. P ni moja ya wasanii matajiri sana Afrika, utajiri wake umechangiwa sana wakati akiimba na kaka yake kwenye kundi lao la P Square. Peter Okoye ndio jina lake halisi, ni mtunzi, mwandishi, mtumbuizaji na pia ni mwandazi wa muziki. Moja ya magari anayomiliki ni 2 Range Rovers ($100,000 – $164,000), BMW X6 ($47,000 – $56,000), Dodge Challenger ($21,600 – $44,000), Porsche 718 Cayman ($21,600), Mercedes AMG GL63 ($90,000), Bentley Mulsanne ($250,000), Jeep Wrangler ($25,200).