Wasanii watano (5) waliowahi kuteswa na mikataba mibovu ya ‘Record Labels’

HomeBurudani

Wasanii watano (5) waliowahi kuteswa na mikataba mibovu ya ‘Record Labels’

Stori kubwa kwa sasa kwenye hapa nchini Tanzania ni msanii Harmonize a.k.a Konde Boy kutema nyongo yote juu ya aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz pamoja ya lebo yake ya WCB.

Harmonize amesema kuwa amekaa kimya kipindi kirefu sana akitunza heshima ya waajiri wake wa zamani, lakini hivi sasa maji yamemfika shingoni kutoka na kile anachodai kuwa upande wa WCB akiwemo bosi wao, wanamtumia watu kumchafua na kumtukana kitu ambacho kinampa ghadhabu sana Harmonize hadi kutapika nyongo hiyo.

Wasanii wafuatao wamewahi kutoka katika mikataba ya record labels kutoka na mikataba hiyo kuwa ya kinyonyaji

1. Lil Wayne na Cash Money Records
Tetesi za ugomvi kati ya Lil Wayne na Birdman zilianza kusikika 2014, Lil Wayne baadae akafungua kesi na madai ya dola milioni 51 dhidi ya Birdman na label ya Cash Money.
Wayne alifungulia Cash Money mashtaka ya kukiuka masharti ya mkataba na pia kuzuia album yake ya 12 ambayo Wayne aliishanya mwenyewe (The Carter V). Mashtaka hayo baada ya muda yalihamishiwa kutoka New York na kufunguliwa New Orleans 2015.

Lil Wayne alifungua mashtaka mengi dhidi ya Birdman na Universal Music Group, kwani Licha ya wasanii kama Drake, Nicki Minaj na Tyga kuwa chini ya Wayne kwenye label ya Young Money, bado Birdman alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha fedha akishirikiana na Universal Music group. Bifu yao ilikuwa kubwa sana hadi 2018 ambapo Birdman kumua kuachia Album ya Carter V itokea kwa gharama ya dola milioni 8 ambapo Lil Wayne alitoka rasmi chini ya Label ya Cash Money

2. Snoop Dogg na Death Row Records
Snoop aliingia dili ya record label ya Death Row mwaka 1992 na akafanikiwa kuwa msanii mkubwa sana katika kiwanda cha muziki wa hiphop duniani baada ya kutoka na wimbo wake wa Doggystyle
mwaka 1993. Mwaka 1997 Snoop alianza kuyumba na kuingia mgogor na label baada ya Dr Dre kuondoka, 2 Pac kufariki pamoja na CEO wa Suge Knight kufungwa gerezani. Baada ya hapo Snoop
alianza kuishutumu label ya Death Row kwa kuzuia malipo ya kazi zake na pia kumnyima haki zake za msingi anazostahili kupata kwenye muziki. 1998 Snoop alitoka Death Row na kujiunga na
No Limit Records ambapo hapo alitoa album 3.

3. Wiz Khalifa na Rostrum Records
Wiz Khalifa alifungua kesi dhidi ya bosi wake aliyepita Benjy Grinberg katika jitihada za kujitoa kifungoni katika mkataba aliowahi kusaini tangu 2005 akiwa na miaka 16. Wiz Khalifa alifungua kesi kudai marupu rupu yake kutoka kwenye label hiyo kwani ambayo amedumu kwa miaka 10 na pia kufungua madai ya dola milioni 1 kama gharama zake za kuendesha kesi.

Khalifa alifungua kesi akidai kuwa Grinberg alifaidika sana kifedha kupitia jina la Wiz Khalifa katika biashara nyingi tu kuliko mwanamuziki ambaye ni Wiz Khalifa. Wiz Khalifa aliachana rasmi ya Grinberg machi 2014.

4. Dr. Dre na Ruthless Records
Hii ni moja ya bifu kubwa sana katika historia ya muziki wa hip hop Marekani kati ya msanii na Record Label. Mwaka 1991 Dr. Dre alipambana sana kuachana na Record label yake ya
Ruthless Records. Drek alisaini mkataba wa kuandaa muziki, yeye hakuwa mtu wa kuimba bali muandazi tu muziki (Producer). Dre alitengeneza albums mbili, kisha kuanza kuhoji
kuhusu vipengele vya mkataba wake na kuanza kuomba madai ya kuondoka kwani haelewi vipengele vya mkataba.

Mabosi wa Ruthless Records Jerry Heller na Easy E walikataa kabisa Dre kuondoka had Dre akaamua kumtafuta Suge Knight na kumuomba amsaidie kung’atuka. Bado haijulikana
Suge Knight na kina Easy E walikubaliana nini, lakini mwaka uliofuata Dre aliachiwa huru na Ruthless na mwaka 1993 yeye na Suge Knight wakafungua Record label ya Death Row.

5. Lil Uzi Vert na Generation Now
Uzi ameingia katika mgogoro na Record Label yake ya Generation now mara kadhaa. Uzi alisaini dili mwaka 2015, akatoka na mixtape ya kwanza mwaka 2016 Lil Uzi Vert vs the World
lakini utata mkubwa ukazuka baada ya ghafla kusambaa taarifa kwamba amesaini dili jingine na Tylor Gang chini ya Wiz Khalifa, ambapo sakata hili lilikataliwa na CEO wa
Generation now, DJ Drama kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mwaka 2017 Uzi akatangaza album yake ya kwanza Luv is Range 2 kukamilika, lakini Album hiyo ikaja kutoka 2017 na Uzi kushutumu uwecheleshwaji wa makusudi wa kuachia Album yake uliosababishwa na label yake. Licha ya migogoro lukuki na label yake, lakini Uzi bado anafanya kazi na Generation Now, anaonekana si mwenye furaha kutoka na kifungo cha mkataba wa kampuni hiyo tangu 2016.

error: Content is protected !!