Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ameadhibiwa na Bunge baada ya kukutwa na hatia ya kulidharau na kuhususha hadhi ya Bunge. Askofu Gwajima ametakiwa kutohudhuria mikutano ya Bunge miwili mfululizo huku Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa naye akikumbana na adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge na kuondolewa kwenye uwakilishi wa Bunge la Afrika (PAP).
Baada ya maamuzi hayo ya Bunge, watu mbalimbali wametoa maoni kupitia mitandao ya kijamii, na haya ni baadhi tu;
Gwajima ni mpinzani
— Nuru (@Nuru75864243) August 31, 2021
Gwajima na Jerry
Heshima ya #bunge
ni muhimu
⚖️✍️✍️????— Official Internationale21 (@OfficialI_Int21) August 31, 2021
Adhabu ya kutohudhulia vikao vya bunge kwa gwajima ni adhabu dhidi ya wananchi anao wawakirisha.
— komamanga (@zedy2004) August 31, 2021
Bunge la leo kiini ni Gwajima.
— Control Quality (@ControlQuality2) August 31, 2021
Natamani sana bunge linapochukua hatua ya kuadhibu wabunge basi wapate muda pia wa kutoa ufafanuzi wa yale wabunge wamekosea. Mf, mbunge wangu @JerrySilaa kama amesema uongo je ukweli wabunge wanakatwa kodi zote? Gwajima kama chanjo ni nzuri si aliomba debate na serikali?
— Hancy Machemba ?? (@hancymachemba) August 31, 2021
Bunge letu cku ya leo limeamua kutumia dakika zaidi ya 200 kumchamba gwajima ?, so sad
— Ibrahim mongomongo (@IMongomongo) August 31, 2021
Safi Spika Ndugai. Anasema wao wamenawa kuhusu Gwajima, kama akiendelea watamwita Waziri wa Ulinzi, Mwanasheria Mkuu kwenye Kamati…. na kwamba ameshangazwa na IGP Sirro kuacha kumchukulia hatua Gwajima hadi apelekewe statement na Waziri.
Spika Ndugai is very BOLD. ??
— Suphian Juma (@SuphianJuma) August 31, 2021
Kwani bunge la leo lilikuwa linahusu mada gani? Maana kila mda nilikuwa nasikia jina la gwajima tena kwa ukali mno ??
— Javan✍ (@StewardJavan) August 31, 2021
Jambo la muhimu ni kuwa Gwajima anaamini ni mkubwa kuliko Bunge na Chama chake, majibu tutayapata jumapili
— TONY ALFRED (@tonyalfredk) August 31, 2021
Jambo la muhimu ni kuwa Gwajima anaamini ni mkubwa kuliko Bunge na Chama chake, majibu tutayapata jumapili
— TONY ALFRED (@tonyalfredk) August 31, 2021
Ila Gwajima Mbabe sana eti anawatishia Kamati ataendelea kusema akiwa nje ya Bunge, ndani ya Bunge kwenye madhabahu na atasema hata akiwa Juu ya DARI.
??
— Sisimizi (@Sisimizi3) August 31, 2021