Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera,Uratibu na Shughuli za Baraza la Wawakilishi) Hamza Hassan Juma, amesema mchakato wa muda wa ajira kwa makarani na wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 umeanza na ailimia 50 ya nafasi hizo ni kwa wasio na ajira.
Fursa hiyo imegawanya katika makundi yote, kwani asilimia 30 ni maofisa kutoka seriklaini, asilimia 20 walimu na ailimia 50 kwa vijana wasio na ajira.
“Mchakato huo utahusisha ngazi zote za kiutawala, ili kuhakikisha wanapatikana makarani na wasimamizi wenye sifa stahiki. Pia wale ambao watakaofanya kazi katika maeneo yao wanayoishi,” alisema.
Baada ya kuwepo kwa taarifa za malipo ya waombaji wa kazi hiyo, Waziri Hamza aliweka wazi kwamba ajira hizo hazitahisisha malipo yoyote kwa muombaji wa ajira na mchakato wa kuchambua maombi ya kazi pamoja na usaili utasimamiwa na kamati maalumu itakayoundwa katika ngazi za kila wilaya.
“Usaili utafanyika katika ngazi ya wilya kwa baadhi ya nafasi za wasimamizi na katika ngazi ya shehia kwa makarani na wasimamizi wa maudhui,” alisema Waziri Hamza.