Watu wanne wamefariki ajali ya treni Tabora

HomeKitaifa

Watu wanne wamefariki ajali ya treni Tabora

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linataarifu umma kuwa Treni ya abiria namba Y14 injini namba 9019, iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, imepata ajali majira ya saa 5:00 asubuhi eneo la Malolo mkoani Tabora Juni, 22,2022.

Treni iliondoka Stesheni ya Kigoma majira ya saa 2 usiku, siku ya Jumanne tarehe 21 Juni 2022, kuelekea Dar es Salaam ikiwa na behewa 8 zilizobeba abiria 930. Ilipofika eneo la Malolo (Km 10 kutoka stesheni ya Tabora) behewa 5 za abiria daraja la tatu, behewa 1 la vifurushi, behewa 1 la huduma ya chakula na vinywaji na behewa la breki zilianguka na kusababisha ajali.

Majeruhi 132 tayari wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa , Kitete- Tabora, kwa ajili ya matibabu na wanaendelea vizuri. Ajali imesababisha jumla ya vifo 4 wakiwemo watoto 2 wakike wenye umri wa miaka 5 na wkaiume miezi 4 na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke.

Shirika liaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam.

Aidha, Shirika la Reli linaendelea kufuatilia kwa karibu, kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua.

error: Content is protected !!